HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba wametoa taulo za kike jozi 1,300 zenye thamani ya shilingi Milioni tatu kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi kupitia mapato ya ndani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed akizungumza mara baada ya kuwakabidhi walimu taulo hizo ametoa rai kwa wadau wengine kuweza kujitokeza kwa kuwasapoti wanafunzi ambao wanakabiliana na changamoto ya ukosefu wa taulo za kike.
“Nitoe wito kwa wadau kujitokeza kuwasapoti wanafunzi na walimu ambao nimewakabidhi taulo hizo hakikisheni mnazigawa kwa wanafunzi ili waweze kutimiza lengo lililokusudiwa”.
Hata hivyo kwa Shule za Sekondari wanafunzi wenye uhitaji ni 1886 ikiwa dazani 55 sawa na jozi 880 zimetolewa na Shule za msingi zimepelekwa dazani 26 sawa na jozi 420.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 9,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa