MKUU wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewaagiza watendaji kuhakikisha ifikapo Februari 27,2024 kufuta suala la kuzungumzia wanafunzi waliopangiwa kuripoti Shuleni Januari 2024 linafika tamati.
Hayo amezungumza katika kikao kazi cha Wakuu wa Shule,Maafisa Elimu,Watendaji Kata na Vijiji kilichofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Madaba day.
Aidha Mkuu wa Wilaya amewaagiza Wakuu wa shule kusimamia Kilimo cha Maharage Lishe aina ya Jesca na mahindi lishe yaliyotolewa kwaajili ya kuzalisha Mbegu mashuleni.
“Niwaombe mbegu mlizopewa hakikisheni mnazalisha ili wapate na shule zingine na tuweze kutokomeza udumavu kwa watoto”.
Katika kikao hicho Ndile amewaagiza walimu hao kuhakikisha wanalima bustani za mbogamboga na matunda ili kuhakikisha wanafunzi wanakula chakula bora na kuwa na afya njema ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
Hata hivyo Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Madaba Maternus Ndumbaro amesema wanafunzi waliopangiwa kujiunga kidato cha kwanza Januari 2024 walikuwa 1254 walioripoti hadi kufikia sasa 1048 wasichana 506 na wavulana 542 sawa na asilimia 83.55.
Upande wa Elimu Msingi darasa la awali wameripoti wanafunzi 1797 sawa na asilimia 100.11 na darasa la kwanza hadi kufikia sasa wameripoti 1749 sawa na asilimia 99.94.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 7,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa