MKUU wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema amewaagiza Watendaji kutoa taarifa kila jioni kwa Mkurugenzi kujua idadi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza walio ripoti shuleni.
Hayo amesema katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya pili ya mwaka 2022/2023 kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Madaba kuhakikisha Madiwani na watendaji wanatoa ushirikiano katika zoezi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema akiwa mgeni rasmi katika Baraza hilo la Madiwani amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri,wataalam na viongozi wa Chama kwa kusimamia miradi ya ujenzi wa madarasa 96 kwa Wilaya ya Songea.
Pololeth kupita pongezi hizo za ujenzi wa Madarasa ametoa rai kwa viongozi wote na wazazi kuhakikisha vijana wote walio faulu na kupangiwa katika shule hizo waweze kujiunga na shule hizo na kuanza masomo mara moja.
“Nimefanya ziara katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea pia nimepata taarifa katika Halmashauri zetu zote tatu bado kuna wanafunzi wapo majumbani hatuna taarifa nao”.
Amesema kuna uwezekana wa wengine kujiunga katika Shule binafsi laki bado kuna utaratibu wa uhamisho ikiwa kuna sheria ya Elimu ambayo ni haki ya mtoto kupata Elimu.
Hata hivyo ameagiza Watendaji Kata na vijiji kuhakikisha wanawasaka vijana wote ambao wanatakiwa kuwepo Darasani kuanzia Januari 9,2023 na kufikia siku 11 tangu kufunguliwa kwa shule.
“ Hapa nazungumzia vijana wa awali,darasa la lakwanza na kidato cha kwanza ambao waliandikisha kwa zaidi ya asilimia miamoja tunataka vijana hawa wawepo darasani mara moja”.
Amesema Serikali ya awamu ya tano imewekeza fedha nyingi kuhakikisha watoto wanasoma katika mazingira mazuri hivyo ni wajibu wa kila kiongozi au mtumishi wa umma asimamie haki za vijana.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed katika Baraza hilo ametoa rai kwa wazazi kuhakikisha watoto wote wanaripoti shuleni na ikiwa ni haki yao ya msingi.
“Watendaji wangu wa Kata pamoja na Maafisa Elimu tuhakikishe kwamba tunatembea nyumba kwa nyumba kufuata ratibu ya uandikisha na wale wanafunzi walioandikishwa “.
Hata hivyo amesema shule nyingi zimefunguliwa ikiwemo shule ya Joseph Kizito Mhagama na imeanza kutoa huduma, miundombinu ipo ikiwa milioni 250 zimetolewa kwaajili ya ujenzi wa Madarasa hivyo, wazazi wahakikishe watoto wanaripoti shuleni kwa wakati.
“Hivyo tutawafuatilia kwasababu Mh. Rais ametoa fedha kuhakikisha tunajenga miundombinu , tunawahimiza wazazi kuhakikisha watoto wenu wanafika shuleni sisi tumejipanga pamoja na idara yangu ya Elimu kuhakikisha tunawapokea watoto hao ili wafanye vizuri katika Mkoa wetu wa Ruvuma na Kitaifa”.
Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Maternus Ndumbaro ametoa takwimu ya wanafunzi wa kidato cha kwanza walioripoti shuleni kufikia Januari 19 ,wavulana 240 na wasichana 265 jumla 535 sawana asilimia 42.2 ikiwa wanafunzi waliopangwa kujiunga na kidato cha kwanza katika Halmashauri ya Madaba wavulana 631 na wasichana 638 jumla 1269.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Januari 20,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa