MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile ametoa rai kwa wataalam Halmashauri ya Madaba kutoe Elimu ya Lishe kila inapokuwa mikutano ya hadhara katika vijiji.
Hayo amesema alipofungua kikao cha utekelezaji wa afua za Lishe cha robo ya nne 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Ndile amesema elimu hiyo ya Lishe pia itolewe kwa Walimu na Wazazi kuhakikisha wanafunzi wanakunywa Maziwa kwa wingi na kuhakikisha wanapata chakula bora wakiwa Shuleni na Nyumbani.
“Wataalam Hakikisheni Mkakati wa mikutano ya vijiji inapofanyika hakikisheni mnakuwepo kuhamasisha na kutoa elimu ya Lishe kwa wananchi”
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya amemwagiza afisa Elimu Msingi na Sekondari kufufua Elimu ya kilimo cha kujitegemea mashuleni ili kuhakikisha chakula na matunda vinapatikana kwa wanafunzi.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Julai 15,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa