MKUU wa Wilaya ya Songea Pololeth Mgema amezindua upandaji wa Miti na kugawa kwa wananchi katika Kijiji cha Lilondo Kata ya Wino Halmashauri ya Madaba.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mgema ameelezea umuhimu wa uwepo wa miti katika mazingira inasaidia katika kuleta hewa safi oksijeni na kunyonya hewa ya kabonidayoksaidi ambayo ni hewa chafu anayotoa mwanadamu.
“Sisi na Miti ni marafiki mmoja akikosekana mwingine hawezi kuishi atakufa kwasababu ya hewa tunayobadilishana “.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya amesema Dunia ipo katika janga la ukame ambalo linasababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo,ufugaji ukataji wa kuni,mkaa na mbao.
Amesema uwiano wa ukataji miti na upandaji wa miti kila mwaka haulingani kwa sababu miti inayopandwa ni michache kutokana na ukataji miti na inayopandwa ni michache.
“Serikali zote Duniani kila mwaka inakutana kwenye mkutano wa mazingira kujadili namna ya kuikarabati dunia iweze kuwa mahali pakuishi”.
Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amewapongeza wananchi hao kwa kujitokeza katika kupanda miti siku ya Januri 1 ikiwa ni siku ya sikukuu
Amesema zoezi hilo la upandaji wa miti limeanza tangia Desemba 31 katika Hospitali ya Wilaya na miti iliyopandwa ni 500 na eneo la Shule ya Lilondo 500 jumla imepandwa 1000.
Mohamed ametoa wito kwa wananchi kufika katika ofisi ya Halmashauri na kuchukua miche ya kupanda katika maeneo yao na vyanzo vya maji na kuhakikisha miti hiyo inatunzwa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Madaba
Januari 1,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa