Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kuacha kuuza ufuta kwa bei ya hasara kwa watu binafsi.
Hayo amezungumza alipoongea na wananchi wa Kata ya Matumbi kijiji cha Ifinga mara baada ya kusikiliza kero za wananchi kulalamikia vyama vya ushirika kucheleweshewa fedha zao.
“Ufuta umeuzwa kwa shilingi 3800 songea vijijini siku mbili zilizopiata kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani walanguzi acheni kuwalaghai wananchi”
Mkuu wa idara ya kilimo Jeseph Mrimi amewapongeza wanchi wa Ifinga ikiwa katika Halamshauri ya Madaba Ifinga wanaongoza kwa uzalishaji wa zao la Ufuta.
Mrimi amesema kwa kipindi chote walikuwa wanahudumiwa na chama cha AMCOS Wino hivyo wameweza kufungua chama chao ambaco watajitegemea na watajisimamia wenyewe.
“kwa kipindi chote ambacho walikuwa wakiuza kupitia Wino AMCOS wamejifunza mengi na changamoto wameziona , mwaka huu mtaanza kujitegemea kupitia chama chenu.
Mrimi amemtaka Afisa maendeleo wa Kata hiyo kufika ofisini kwake ili kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri utakaosaidia kuanza kwa chama hicho cha ushirika”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Juni 4,2023
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa