• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

DC Ndile awataka watumishi kuwatumiakia wananchi kwa weledi

Posted on: March 29th, 2023

MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile ameongea na watumishi Halmashauri ya Madaba kwa mara ya kwanza ikiwa ni siku ya tatu kuanza kazi mara baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas.

Akizungumza na watumishi hao katika ukumbi wa Halmashauri ya Madaba amesema watumishi ni mali ya Serikali wahakikishe wanawatumikia wananchi ipasavyo ili wananchi waweze kufikia malengo yao.

“Serikali inajua mnastahiki zenu haiwezi kuwaacha kwa kuwapandisha madaraja na kuwaongezea mishahara hata mkistaafu mpewe na peshion, Serikali inajua mnawatumikia wananchi lazima muwe katika mazingira mazuri”.

Hata hivyo Ndile amesema ameletwa Wilaya ya Songea kwaajili ya kusimamamia maelekezo ya Serikali kama inavyotaka ikiwa kila jambo litafanyika  kama itakavyoelekezwa.

“Serikali imeelekeza kuhusu Elimu Watoto wa awali wanaandikishwe,darasa la kwanza pamoja na anayemaliza darasa la saba aende kidato cha kwanza kazi yangu mimi ni kusimamia”.

Amesema hayo yote yatafanyika vizuri kama kutakuwa na ushirikiano na wazazi,walimu na viongozi wengine ili kila idara iweze kufanya vizuri ikiwa kwa upande wa Madaba Elimu imefanya vizuri.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed akisoma taarifa kwa Mkuu wa Wilaya amempongeza kwa kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea na atahakikisha anapewa ushirikianao na watumishi wa Halmashauri hiyo ili kuhakikisha miradi inayoletwa na Serikali inakamilika kwa wakati.

Mohamed amesema Halmashauri imekuwa inategemea mapato kupitia kilimo pekee  kwa sasa imepata wawekezaji wa uchimbaji wa makaa ya mawe katika Kata ya Mtyangimbole ambao wanatarajia kuanza Machi 2023

Amesema   Halmashauri hiyo inasimamia na  kutekeleza miradi mbalimbali  ya maendeleo hivyo ipo  iliyokamilika na    mingine inaendelea kutekelezwa.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa