Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile, Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Madaba,wataalam na wenyeviti wa Vijiji Mkoa wa Ruvuma wamefanya ziara ya kujifunza juu ya Utunzaji wa Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa.
Katika ziara hiyo wametembelea kiwanda cha Dazhong Wood kinachotengeneza marine board na plywood kwa kutumia magogo ya miti yanayobaki baada ya kuvuna miti.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amesema katika ziara hiyo wamejifunza ikiwa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba wanavunamiti na mabaki ya magogo hayo yanakuwahayana kazi yoyote.
“Kumbe magogo ya miti yanaweza kutengenezwa na kutoa bidhaa ambazo tunazitumia kila siku hata Madaba inawezekana tukapata Kiwanda”.
Ndile baada ya kutembelea na kujifunza amewakaribisha wawekezaji hao kuwekeza Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ikiwa kuna mashamba ya miti na mazao hayo yanapatikana kwa urahisi.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa