MKUU wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile ametoa rai kwa waratibu wa Lishe kuendelea kutilia mkazo juu ya utoaji wa elimu ya lishe kwa wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
Hayo amesema katika kikao cha tathimini ya utekeleza wa mkataba wa lishe kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024 katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
“Tukiwawezesha akina mama wajawazito wakiwa na afya nzuri watoto wanaozaliwa watakuwa na afya njema wakizaliwa chini ya uzito hawewezi kuwa na afya njema tunaweza kuwa na Taifa ambalo hakili zao siyo nzito ya kufikili”.
Hata hivyo kapenjama amesema nchi ya Tanzania inahangaika na mambo matatu kuondoa ujinga,umaskini na magonjwa ikiwa ni hali mbaya ambayo inaathiri afya ya mwanadamu.
Serikali inahangaika kujenga Hospitali nyingi sana lengo kupunguza vifo ,mtu akiugua mara kwa mara anaweza kuishi kwa mda mfupi,kama watu wamezaliwa na afya ya mgogoro hawawezi kuwa na afya nzuri”
“Natoa rai kwa wanaume kuhakikisha wanawake wajawazito wanakula vizuri ili waweze kuleta watoto wenye hakili miaka ya zamani wajawazito walikuwa hawatakiwi kula mayai ktokana hakukuwa na hospitali za kutosha lakini kwa sasa kuna hospitali ambapo mjamzito anaweza kusaidiwa na kujifungua kwa oparetioni”.
Ndile amesema wananchi wa halmashauri ya Wilaya ya Madaba waendelee kuchangia chakula shuleni ili watoto waweze kusoma vizuri na kufauru katika masomo yao.
“Tumefaulu pakubwa katika halamshauri ya Wilaya ya Madaba watoto wanakula shuleni Afisa elimu endelea kusimamia hili”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 28,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa