MKUU wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile ameogoza zoezi la upandaji wa Miti 50 ya Matunda aina ya Parachichi katika Shule ya Sekondari ya Lilondo iliyotolewa na Wakala wa Shamaba la Miti Wino Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Akizungumza mara baada ya upandaji wa miti hiyo Ndile amewapongeza walimu na wanafunzi kwaajili ya zoezi hilo pamoja na kuweka mazingira katika hali ya usafi.
Mkuu wa Wilaya amesema upandaji wa miti ya matunda mashuleni ni kampeni ya kutokomeza suala nzima la udumavu kwa watoto.
Hata hivyo amewapongea Wakala wa Miti Wino( TFS) Wino kwa kufanya kazi nzuri kwa wananchi bila kujali kuangalia mashamba ya Serikali pekee.
“TFS Wino wanafanya kazi nzuri na mara nyingi nimewaeleza wote wenye mashamba makubwa katika Wilaya ya Songea kama Ndolela,Aviv uwepo wenu lazima uwe na matokeo chanya kwa wananchi TFS ambayo ni serikali wangeweza wasililete chochote lakini kila siku wanajitaidi kutoa miti katika maeneo mengi”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed ameshiriki zoezi hilo ameto wito kwa Walimu na wanafunzi kuilinda na kuitunza miti hiyo.
“Tumefanya hivyo kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata mlo kamili shuleni Mtendaji wa Kata,Kijiji na Mwalimu Mkuu nawaomba msimamie miti na kila mwanafunzi akabidhiwe mti wake na autunze”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 16,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa