MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile ameongea na kujitambulisha kwa wananchi wa kijiji cha Ifinga kata ya Matumbi tangu alipoteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Wilaya.
Kata ya Matumbi ipo takribani kilomita 68 kutoka makao makuu ya Halmashauri na katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ametembelea Shule ya Sekondari Ifinga ambayo inawanafunzi 77 kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne na walimu 8.
Hivyo Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa wananchi wa Kata hiyo kujenga Hosteli ili kuhakikisha wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali wasome katika Shule hiyo.
“Mimi kama Mkuu wa Wilaya Shule hiyo haiwezi kuwa na tija Mwl. Nyerere toka mwanzo alifikilia kujenga utaifa na uzalendo katika nchi hii alitengeneza mikakati mbalimbali Mwanafunzi aliyezalwa Mbinga ataenda kusoma Monduli lengo ilikuwa kuchanganya watoto wa tamaduni mbalimbali”.
Hivyo Mkuu wa Wilaya amesema siyo vema mtoto anaanza chekeckea mpaka anafika kidato cha nne anasoma katika kijiji cha ifinga bila kuonana na wanafunzi wengine kutoka maeneo mengingi.
“Naona siyo vema lazima tubadilike tuipanue shule ili kuleta wanafunzi kutoka maeneo mengine hata kwa kuanza mkondo mmoja ili wale 77 wa hapa wachanganyike na wengine kutoka sehemu mbalimbali ndani ya Wilaya ya Songea anagalau wafike 500 au 400”.
Hata hivyo amemwagiza katibu Tawala wa Wilaya ya Songea kutoa maelekezo kwa Halamshauri ili jambo hilo liwekwe kwenye mipango yao na kuhakikisha mpango huo unakamilika ifikapo Januari 2024.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halamshauri ya Madaba
Juni 3,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa