MKUU wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile amezindua ujenzi wa Soko unaojengwa kwa Shilingi Milioni 190 ,Kijiji cha Lituta Kata ya Lituta Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kupitia Mradi wa TASAF.
Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi huo ametoa rai kwa wananchi kushiriki katika hatua zote zinazotakiwa ikiwa kuchimba msingi,kuweka kifusi pamoja na kusomba maji.
Hata hivyo ameagiza mradi huo mara utakapokamilika wafanyabiashara ambao wamejenga na kutumia Soko la mda wapewe kipaumbele kupewa vizimba vya kufanyia Biashara zao .
Ndile amesema ujenzi huo wa Soko la Kisasa uwekwe wazi ikiwa matumizi ya fedha katika utakao jumuisha ujenzi wa vizimba, Matundu ya vyoo 6 pamoja na guba ikiwa ni Soko la kisasa.
“Mkiona Soko linakuja la shilingi Milioni 190 katia Kijiji chenu Madaba kuna vijiji 22 hapa ndio mji ,ndiomana Serikali imeona mletewe Soko la Kisasa na miundombinu mingine”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Septemba 13,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa