MKUU wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewaagiza watendaji Kata kutoa Elimu katika siku maalumu za Lishe kwa kubadilishana Kata ili kutilia mkazo katika Jamii suala la Lishe.
Akizungumza katika kikao cha tathimini ya Lishe kilichofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba amesema uzolotaji katika elimu ya kujitegemea Mashuleni zipo nyuma.
“Naelekeza ili kuboresha lishe kwa watoto wetu kuanzia chekechea hadi Sekondari Elimu ya Kujitegemea ipewe kipaumbele lazima bustani za shule ziimarishwe”.
Ndile amesema kwa asilimia kubwa Halmashauri imefanikiwa zoezi la wanafunzi kula Shuleni lakini siyo kwa kiwango cha kula chakula bora hivyo amesema kila shule ihakikishe inalima mboga mboga katika maeneo ya Shule ili iweze kusaidia watoto.
“Mboga za majani na matunda zikikosekana katika Mwili wa binadamu kwa upande wa lishe tutakuwa hatujapiga hatua, watoto hawawezi kufauru mitihani kama wanaudumavu”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 5,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa