AFISA Ustawi wa Jamii John Mashauri wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba ametoa elimu ya kujiunga na Bima ya iChF nafuu kwa vibarua wa Shamba la Miti Wino.
Akizungumza na vibarua hao katika awamu tofauti amesema kuwa Bima ya iChF inagharimu kiasi cha shilingi Elfu 30,000/= kwa Mwaka na kujumuisha watu sita katika Familia
“Ni mfumo ambao umewekwa katika Mkoa wa Ruvuma ilikuhakikisha kila mwananchi anapata matibabu ya gharama nafuu”.
Hata hivyo amesema ukijiunga na Bima hiyo inatumika kwa mda wa mwaka mmoja na inachukua nafasi kubwa ya wategemezi Baba mama na watoto na kupata matibabu katika Vituo vyote vya Afya katika Mkoa wa Ruvuma.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Agosti 26.2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa