Mwenyekiti wa Halamshauri ya Madaba Teofanes Mlelwa amemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama katika Hafla ya Mahafari ya Kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Magingo Kata ya Mkongotema Halmashauri ya Madaba.
Mlelwa amewapongeza wananchi na uongozi wa Kijiji kwa kuanzisha Shule hiyo kupitia nguvu za wananchi na Serikali kuendeleza kuboresha Miundombinu mbalimbali katika Shule hiyo.
Mkuu wa Shule amezitaja changamoto zinazopatikana katika Shule hiyo ikiwemo ukosefu wa Jengo la Utawala,Bweni la wasinana na wavulana,upungufu wa Nyumba za Walimu zikiwemo Nyumba 16 na zilizopo ni 2 pamoja na ukosefu wa panzia za madarasa ambayo wanafunzi wanatumia kulala.
Afisa Elimu Sekondari Taaluma Devis Mwasi akijibu changamoto hizo amesema bweni lililojengwa kupitia nguvu za wananchi na mfuko wa jimbo wataandika andiko maalumu kupitia bajeti ya mwaka wa Fedha 2024/2025.
“Niseme tu kwenye mpango wa bajeti 2024/2025 pamoja na bajeti ya kawaida tutaomba ombi maalumu kwaajili ya ukamilishaji wa hosteli ya Magingo Sekondari itakamilika na wanafunzi wetu wataishi mahali pazuri zinahitajika Milioni 80”.
Hata hivyo Mwenyekiti ametatua changamoto ya mapazia kwa kuchangia kupitia keki na kupatikana zaidi ya shilingi laki 5.
Kutoka Kitengo cha Mawasilino Halmashauri ya Madaba
Septemba 28,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa