KIKAO maalum cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Madaba limepitisha mpango wa bajeti ya barabara kwa miradi ya matengenezo na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Akisoma taarifa hiyo Kaimu Meneja wa TARURA Saimon Binamu amesema mpango huo unalenga kuboresha barabara zilizopo na kusaidia maeneo yote wakati wote kwa muunganiko wa huduma za usafi wa Barabara ndani ya Halmashauri kwa shilingi Milioni 631,840,000/=.
“Mapendekezo ya bajeti hii umezingatia maelekezo yaliyomo kwenye mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025 uliotolewa Disemba 2023”.
Binamu amesema vigezo vya kibajeti vimetumika kupitia mfumo wa uratibu wa mtandao wa barabara unaosimamiwa na TARURA ambao unazingatia aina ya barabara inayounganisha nyingine zenye watumiaji wengi,maeneo yenye huduma za kijamii,uzalishaji wa mazao pamoja na maeneo ya vitega uchumi.
“Mpango huo utazingatia kuhusisha matengenezo ya kawaida kilomita 12.7 maeneo kolofi kilomita 6.70,matengenezo maalumu kilomita 13.0,vivuko 17,makalavati 10,madaraja ya ufuto 4 kwa shilingi Milioni 631,840,000/=”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 8,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa