Katika mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba imepanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni 2 katika matengenezo ya Barabara.
Hayo ameyasema kaimu Meneja wa Wakala wa barabara vijijini (TARURA)
Godfrey Mngale katika kikao cha Baraza la Madiwani kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Hata hivyo amesema Halmashauri imepanga kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 613 kwa matengenezo ya mtandao wake wa barabara,matengenezo ya kawaida ikiwa fedha zilizotengwa kiasi cha shilingi milioni 12 ambazo zinatarajia kufanya matengenezo yenye jumla ya kilomita 3.0
Amesema sema matengenezo sehemu kolofi fedha zilizotengwa kiasi cha shilingi milioni 186 ambazo zinatarajia kufanya matengenezo ya kilo mita 2.2 pamoja na matengenezo maalumu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 415 ambazo zinatarajia kufanya matengenezo yenye jumla ya kilomita 22.79.
Mngale amesema milioni 500 zimetengwa kwaajili ya barabara za changarawe kilomita 44.7,bilioni moja ambayo inatarajia kujenga barabara ya Lami yenye kilomita 1.5 pamoja na daraja na matengenezo ya barabara kilomita 3.5.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Olaph Pili amempongeza Mbunge wa jimbo la Madaba kwa kuhakikisha bajeti ya matengezo ya Barabara inapatikana.
Pia Pili amewapongeza wataalamu wa TARURA pamoja na watumishi wote wa Halmashauri inayoongozwa na Mkurugenzi mtendaji Sajidu Idrisa Mohamed kwa utendaji kazi na kuhakikisha Halmashauri ya Madaba inafunguka kwa maendeleo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Madaba
Februari 13,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa