MWENYEKITI wa Halmashauri ya Madaba Theophanes Mlelwa amefanya mkutano na wananchi wa Kata ya Lituta kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuhakikisha zinatatuliwa.
Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti ameelezea namna ambavyo Serikali ya awamu ya sita inavyotatua changamoto hizo kwa kuhakikisha Madaba inakuwa na Barabara,Maji , upatikanaji wa Mbolea za Ruzuku pamoja na huduma zingine nyingi kwa wananchi hao.
“Seikali ya Rais Samia pamoja na Mbunge wetu Joseph Mhangama wanatupenda madaba wamehakikisha kila mtaa barabara zimechongwa na kutoka Halmashauri mpaka Hospitali ya Wilaya itatengenezwa kwa kiwango cha lami”.
Meneja wa TARURA Wilaya ya Songea John Masatu akizungumza katika mkutano huo amesema Serikali ya awamu ya Sita imejikita kuboresha mji wa Madaba hasa kata ya Lituta kwa upande wa miundombinu.
Amesema mwaka wa fedha uliopita 2021/2022 kwa kushirikiana na uongozi wa Halmashauri walijikita kufungua Barabara zote za Kata ya Lituta.
Masatu ameeleza changamoto zilizojitokeza katika ufunguzi wa Barabara hizo ikiwemo katika ujenzi wa Madaraja na Makaravati lakini yamekamilika na zimeanza kutumika.
“Serikali inampango maalumu Barabara zote zilizokuwa zinasumbu katika kipindi cha masika zinawekewa kifusi cha changalawe”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Madaba
Novemba 20,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa