HALMASHAURI ya Madaba imepanga kukusanya na kutumia zaidi ya shilingi bilioni 12 kwaajili ya Maendeleo mwaka 2021-2022.
Akitoa taarifa ya mafanikio ya mwaka 2019-2020 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Kassim Mpenda amesema imetokana na usimamizi na elimu inayotolewa kwa watu wanaolipa ushuru na kodi mbalimbali.
Mpenda amesema usimamizi wa fedha umeendelea kuimalika kutokana na mifumo inayoongoza na ufanyanyaji kazi wa mfumo wa udhibiti wa fedha EPICA ambao unaongoza uwazi na uwajibikaji katika mchakato mzima wa malipo.
Aidha Mpenda amesema Halmashauri kufikia sasa imeanza kutoa asilimia 10 ambayo ni matakwa ya kisheria kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu uliopangwa,ni mafanikio ambayo yamepatikana kwa asilimia 91 ya kadilio la milioni 74 kwa mwaka.
Amesema katika uandaaji wa bajeti wa mwaka 2021-2022 amesema Halmashauri imezingatia miongozo na maelekezo mbalimbali ya Serikali ikiwemo ukusanyaji wa mapato na utendaji wa Rasilimali fedha mpango wa maendeleo ya Taifa wa miaka mitano 2021 mpaka 2025 mpango huo unazingatia vipaumbele vya kisekta kama vile Fedha,Elimu,Mifugo,uvuvi,Afya, uthibibiti wa maji taka,Utalii na Viwanda.
“Halmashauri imezingatia katka uandaji wa bajeti 2021-2022 Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya uchaguzi mkuu 2020 hotuba ya Mh.Rais wa Tanzania na hotuba ya Waziri Mkuu na ziara yake ya tarehe 4 mpaka 7 Januari Mkoani Ruvuma kuzingatia maswala mtambuka kama Magonjwa ya Ukimwi,Maafa,Mazingira na Rushwa,mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini pamoja na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa Mkoa na Taifa”.
Mwenyekiti wa Halmashauri Teofanes Mlelwa wakati akifunga kikao hicho amewataka wataalamu wa Halmashauri hiyo kuzingatia na kufanya kazi aliyoajiliwa bila kuingilia kazi ya mwingine.
“Waheshimiwa Madiwani mkafanye kazi kwa bidii pamoja na kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao,Bajeti mmeipitisha zaidi tunahitaji ushirikiano katika utendaji”.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Machi 12,2021.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa