MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge amehamasisha wananchi ifikapo Agasti kujitokeza kuhesabiwa.
Hayo amesema katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,kimkoa imefanyika katika Halmashauri ya Mdaba Wilaya ya Songea na ameeleza faida ya Sensa ya watu na makazi.
Amesema zoezi hilo litawezesha Taifa kupanga mipango ya Maendeleo ya mda mfupi na mrefu kwa mstakabali ya maisha ya wananchi zoezi hilo linaendelea na uwekaji wa anwani za makazi na postikodi ili tuwe na uhakika wa kufanikisha sense ya mwaka huu.
“ Niwakumbushe kuwa mwa huu tunafanya sensa ya watu na makazi Hivyo niwahimiza wananchi wote kujitokeza kuhesabiwa “.
Ibuge katika halfu ya shelehe hizo amesema Serikali ya awamu ya sita imekuwa mstari wa mbele kuwawezesha wanawake kwa njia mbalimbali ikiwemo kupokea fedha kupitia mpango wa Maendeleo kwa Taifa na mapambano Dhidi ya Uviko 19 kwenye sekta ya Afya.
Amesema fedha hizo ni kwaajili ya kujenge majengo matatu ya dharura,Jengo la wagonjwa mahututi moja kwa lengo la kuhakikisha wanawake wajawazito na watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano wanapata huduma nzuri.
Hata hivyo Ibuge amesema katika eneo la kuendelea kujikinga na VVU-UKIMWI janga bado lipo ni jukumu la wazazi na walezi kujilinda na kuelimisha jamii na kujihadhali na janga hili.
Ibuge ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia kwa kusimamia kwa ukaribu wa utoaji wa mikopo isiyo na riba kwa wanawake inayotokana kwa asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akisoma Risala mwakilishi wa Wanawake Mariam Juma amesema Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa Mikoa iliyoathirika na Janga la UKIMWI hivyo wamejiwekea mikakati ya kutoa elimu,kupima afya kwa hiari,kutoa huduma kwa watoto yatima pamoja na kukemea mila na desturi zinazochochea maambukizi.
Ikiwemo kurithi wajane,ngoma za usiku,ulevi uliokithiri,kuendekeza ngono zembe na kutoa msisitizo wa wananchi kubadili tabia zao.
Juma ameeleza changamoto wanazokabiliwa ikiwemo fedha za mikopo zinazotolewa hazitoshelezi kuwapatia vikundi vyote kulingana na uhitaji,Vikundi kutorejesha mikopo kwa wakati pamoja na uelewa mdogo kwa jamii kuhusu elimu ya usawa na jinsia.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Machi 9,2022.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa