MKUU wa Idara ya Elimu Msingi Saada Chwaya ametoa rai kwa wananchi kuandikisha wanafunzi wa awali,darasa la kwanza,MEMKWA pamoj na wenye ulemavu (Wenye mahitaji maalum) kuanzia miaka 5.
Hayo alisema alipozungumza na wananchi wa Kijiji cha Ngadinda Kata ya Gumbiro amesema uandikisha huo umeanza rasmi Oktoba 1,2023 na mwisho wa uandikisha utakuwa Disemba 31,2023.
“Mkiwaandikisha Watoto kwa wingi itawasaidia kupata fedha kwaajili ya ujenzi wa Shule shikizi katika Kata hii ya Gumbiro tunaomba mjitahidi watoto wote wenye umri wa kwenda shule waandikishwe”.
Hata hivyo Chwaya amesema mtoto aandikishwe shule iliyo karibu na anapoishi ili kuepuka kutembea umbali mrefu .
Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza kuwalinda wototo na kuwahimiza kusoma ikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatoa fedha kwaajili ya kuboresha miundombinu ya Shule.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Oktoba 20,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa