AFISA Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Malimi Ndulu ametoa elimu ya kutambua umuhimu wa kupimiwa viwanja na kutambulika kwa hati miliki kwa wananchi.
Hayo amesema katika kikao cha uchaguzi wa Viongozi wa Mahanje SACCOS uliofanyika katika ukumbi wa amani Madaba na kuwapa elimu hiyo ili iwawezeshe kuwekeza dhamana wakati wa kukopa katika Taasisi mbalimbali za kifedha.
“Tumekuwa tukitoa umuhimu wa kuweza kupanga na kupima maeneo ili kumwezesha mkopaji katika taasisi Mbalimbali za Kifedha”.
Ndulu ameelezea faida za upimaji wa viwanja amesema eneo lililopangwa na kupimwa linapanda thamani,kutambulika kwa mmiliki kwa kuandaliwa hati miliki pia husaidia kuondoa migogoro, kutatua changamoto ya kifamilia,kuongeza mapato ya Serikali kila mwaka.
Hata hivyo Afisa Ardhi amesema kwa mwananchi ambaye anahitaji kuchukua mkopo na anaeneo ambalo halijapimwa ofisi ya ardhi wanathibitisha eneo hilo kwa maandishi.
“ Wananchi ambao maeneo yao hayajapimwa tunasisitiza yawe na nyaraka za umiliki bila kufanya hivyo watasababisha migogoro”.
Hivyo afisa Arddhi ametoa rai kwa wananchi ambao maeneo yao yamepangwa na kupimwa na linastahili kuwa na hati miliki waweze kulipia ikiwa kwa sasa gharama zimeshuka kwa viwanja vidogo vidogo vinalipiwa elfu 30,000/= hadi 45,000/= na haipaswi kulipa zaidi ya 120,000/=.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Oktoba 14,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa