MKURUGENZI Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamed amewaagiza watendaji kuanza mara moja ujenzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa ya Christina Mndeme inayotarajiwa kujengwa kwa zaidi ya shilingi Bilioni 3 kupitia fedha za ushuru wa mazao.
Hayo amesema alipotembelea na kugaua ujenzi wa mradi huo unaojengwa Kata ya Gumbiro ambapo kufikia sasa Milioni 169 zimeingia kwaajili ya kuanza utekelezaji.
Hivyo Mkurugenzi ameagiza kila hatua itakayoendelea katika ujenzi huo wananchi washirikishwe na wawepo katika eneo la mrdai.
“Mtendaji ,natoa wiki mbili nione majengo yamesimama, kwasababu tofari zipo hakuna kisingizio fedha ipo,na msiwalazimishe wananchi mtumie lugha laini ya kuongea nao”.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ngadinda Shabani Mandiliku ambaye ni mwenyekiti wa usimamizi wa Mradi huo amesema hadi kufikia sasa mradi umefikia hatua ya ufyatuaji wa tofari na kuchimba msingi.
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Februari 15,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa