• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

WAZIRI Mkuu aagiza Mamlaka za serikali za mitaa kutenga bajeti kuhifadhi maeneo ya kihistoria

Posted on: February 27th, 2021

WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameiagiza mikoa na Mamlaka zote za serikali za mitaa kutenga bajeti ya kuyahifadhi maeneo yote ya kihistoria ili kutopoteza historia yake kwa manufaa ya Taifa.

Majaliwa ametoa agizo hilo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa kwenye kilele cha tamasha la kumbukizi ya miaka 114 ya vita ya Majimaji lililofanyika kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea.

Waziri Mkuu pia ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kuadhimisha kumbukizi hizo ili ziwe sehemu ya vivutio vya utalii nchini ambazo zinachangia kuongeza pato la Taifa na kwamba Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Habari zihamasishe na kuelimisha jamii fursa za kumiliki maeneo ya malikale.

Akizungumzia mashujaa wa vita ya Majimaji ,Waziri Mkuu ameagiza kumbukumbu zilizopo ndani ya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji zinaendelea kuhifadhiwa ili kujenga uzalendo na kuleta utaifa kwa kizazi  kilichopo na kijacho.

“Mkoa wa Ruvuma hivi sasa una makumbusho mawili ambayo ni Makumbusho ya Majimaji na Makumbusho ya Dkt.Hayati Rashid Mfaume Kawawa,Mkoa huu ndiyo kitovu cha kusaidia wanaharakati wa ukombozi wa Afrika hususan nchi jirani ya Msumbiji’’,alisisitiza Waziri Mkuu.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Songea mjini Dkt.Damas Ndumbaro  akizungumzia kumbukizi ya miaka 114 tangu kunyongwa mashujaa wa vita Majimaji,amesema maadhimisho hayo yamelenga kuenzi ushujaa  wa wazee wetu katika harakati za awali za ukombozi dhidi ya wakoloni.

“Maisha ya wazee wetu ni fahari yetu kwa sababu wazee hawa walipigania nchi kwa uzalendo wa hali ya juu,ukombozi wa mwafrika una historia kubwa sana hapa kwa sababu mapambano yaliyofanyika kwa muda mrefu zaidi dhidi ya mkoloni nchini Tanzania yalifanyika Songea’’,alisema Dkt.Ndumbaro.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Christawaja Ntandu  ameyataja malengo ya tamasha la kumbukizi ya mashujaa wa majimaji ambalo hufanyika kila mwaka kuwa ni  kukumbuka na kuwaenzi mababu zetu ambao walinyongwa Februari 27,1906 na kuzikwa kwenye makaburi mawili ndani ya makumbusho ya Majimaji.

Hata hivyo amesema tamasha hilo hutoa fursa kwa wananchi kutunza,kuenzi na kuendeleza uzalendo,amani na mshikamo ambao umerithiwa kutoka kwa mababu zetu na kwamba tamasha hilo pi hutumika kuibua na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ukanda wa kusini.

Naye Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Dkt.Noel Lwoga amesema wazee waliopigana katika vita ya Majimaji miaka 114 iliyopita dhidi ya wakoloni walitoa mchango mkubwa katika kutetea taifa letu na kwamba vita ya Majimaji imebeba utajiri mkubwa wa historia ya ukombozi na uhuru wa nchi yetu.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Februari 27,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa