KATIBU Tawala Mkoa wa Ruvuma Rehema Seif Madenge amewataka Watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Madaba kuweka mikakati ya kutozalisha hoja.
Hayo amesema katika kikao cha mapitio ya utekelezaji wa maagizo ya kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi ya Mkurugenzi.
Madenge amewapongeza watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kujibu hoja zilizoibuliwa kwa usahihi, na ushirikiano.
“ Nasisitiza kukamilisha kujibu hoja zote kwa wakati na hapa nazungumzia kwa hoja zitakazoibuliwa zijibiwe kwa usahihi na ushirikiano hoja hizi sisi tunazizalisha”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba
Aprili 2,2024.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa