• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

TAKUKURU Ruvuma imejipanga kufuatilia fedha za Maendeleo

Posted on: November 15th, 2021

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Ruvuma kwa kipindi cha robo Mwaka Octoba hadi Desemba wamejipanga kufuatilia fedha zilizotolewa na kwaajili ya mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.

Akitoa taarifa hiyo Mkuu wa Takukuru  Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda amesema pamoja na utekelezaji wa robo mwaka wamejiwekea vipaumbele ikiwemo kuendelea kufanya ufuatiliaji katika makusanyo ya fedha za ndani za Halmashauri kupitia utaratibu wa POS.

Mwenda amesema katika kipindi cha miezi 3 ya kumaliza mwaka wataongeza kasi katika kufanya chambuzi za mifumo hasa katika maeneo yanayolalamikiwa zaidi kama maeneo ya utoaji wa huduma kwa wananchi na katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa katika miradi ya sekta ya Elimu,Ununuzi,Kilimo,Afya,Uchukukuzi pamoja na uendeshaji wa vyama vya Ushirika.

“Mkoa wetu ni moja kati ya mikoa iliyopata fedha zilizotolewa kwaajili ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19”.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Ruvuma ametoa rai  kwa wahusika wote waliopewa dhamana ya mabilioni kwaajili ya utekelezaji wa Miradi iliyoainishwa kufuata miongozo sahihi ya matumizi ya fedha hizo.

Mwenda ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kutoa ushirikiano Mkubwa kwa Viongozi katika utekelezaji wa miradi iliyoainishwa kupitia mpango wa Maendeleo wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19.

Hata hivyo Mwenda amesema kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 iliyoanzia Julai-Septemba 2021 TAKUKURU ilifanya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo (PETS)  kumi na tatu yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kubaini mapungufu machache.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka ofisi ya Habari ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma

Novemba 15,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa