• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

SERIKALI yatoa bilioni 3.6 kutekeleza miradi miwili Madaba

Posted on: March 9th, 2021

SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imetoa shilingi bilioni 3.6 kutekeleza miradi miwili katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Kassim Mpenda akizungumza katika mahojiano maalum ofisini kwake mjini Madaba amesema katika mradi wa kwanza serikali imetoa shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kutekeleza mradi wa jengo la Halmashauri.

Mpenda amesema hadi sasa jengo hilo limekamilika kwa asilimia 100 ambapo jumla ya shilingi bilioni 2.914 zimetumika na kwamba mradi  huo umekamilika na jengo limeanza kutumika hivyo kutatua changamoto ya uhaba wa ofisi uliokuwa unawakabili watumishi wa Halmashauri hiyo na wananchi.

“Kwa ujumla wake katika kutekeleza mradi huu wa jengo la utawala,tulipokea shilingi bilioni tatu,mradi ulianza mwaka 2017 na umekamilika  kupitia force akaunti mwaka 2020 kwa gharama ya shilingi bilioni 2.914,tumeokoa shilingi milioni 85  ambazo zimetumika  kununua kiti na meza kwa kila mtumishi,kutengeneza mifereji na kutengeneza sakafu ya tofali za saruji maeneo yote yanayozunguka jengo’’,alisema Mpenda.

Amesema kupitia fedha zilizobakia Halmashauri pia imeweza kununua  kwa ajili ya ukumbi wa mikutano vikiwemo viti,meza vifaa, vipaza sauti na  vifaa vya kuzungumzia(Microphone).

Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Halmashauri ya Madaba ameutaja mradi mwingine ambao unatekelezwa na Halmashauri hiyo hivi sasa ni ujenzi wa nyumba saba za watumishi ambapo serikali imetoa shilingi milioni 600 kutekeleza mradi huo.

Amesema kati ya fedha hizo shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya kujenga nyumba ya ghorofa moja ya kuishi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo na shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya  kujenga nyumba sita za wakuu wa Idara.

Kwa mujibu wa Mpenda kila nyumba ya Mkuu wa Idara inagharimu shilingi milioni 50 na kwamba mradi huo unatekelezwa kwa mfumo wa force akaunti ambapo hadi sasa mradi umefikia hatua nzuri,na unatarajia kukamilika Mei 2021.

“Tunaishukuru sana serikali kupitia Rais wetu Dkt.John Magufuli kwa kweli sisi Halmashauri ya Madaba tumepewa upendeleo wa kipekee nadhani ni kwa sababu Halmashauri yetu bado changa hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kuwa na miundombinu mbalimbali’’,alisema Mpenda.

Halmashauri ya Madaba ni miongoni mwa Halmashauri tatu zilizopo katika Wilaya ya Songea,Halmashauri nyingine ni Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Songea.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari wa Mkoa wa Ruvuma

Machi 9,2021

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MADABA YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024.

    June 19, 2025
  • UJENZI WA MADARASA 2 NA MATUNDU 6 YA VYOO SHULE YA MSINGI KIPINGO WAKAMILIKA KWA ASILIMIA 100

    May 30, 2025
  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa