• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RUWASA Ruvuma ilivyodhamiria kusambaza Maji vijijini

Posted on: February 8th, 2021

Mhandisi Rebman Ganshonga ni Meneja wa RUWASA  Mkoa wa Ruvuma,anabainisha utekelezaji wa miradi ya maji na mwelekeo wa RUWASA mkoani Ruvuma katika utoaji huduma ya maji vijijini.

Mhandisi Ganshonga anataja hali ya upatikanaji huduma ya maji kwa kila Halmashauri hadi kufikia Juni 2019,ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Songea yenye watu 141,427,idadi ya watu wanaopata huduma ya maji ni 86,270 sawa na asilimia 61.0 na kwamba Halmashauri hiyo ina vituo vinavyotoa maji 951 kati ya hivyo vinavyofanyakazi ni vituo 590.

Kwa mujibu wa Mhandisi huyo, katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea RUWASA inahudumia wakazi 90,730,watu wanaopata huduma ya maji ni 45,479 sawa na asilimia 50.0 ambapo idadi ya vituo vya kutolea maji ni 401 kati ya hivyo vituo vinavyofanya kazi ni 372.

“Katika Halmashauri ya Mbinga yenye idadi ya watu 235,648,idadi ya watu wanaopata maji ni 123,648 sawa na asilimia 52.4,idadi ya vituo vya kuchotea maji ni 375,vituo vinavyofanya kazi ni 196’’,anasema Mhandisi Ganshonga.

Kulingana na Meneja huyo,katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo yenye wakazi  226,945,idadi ya watu wanaopata huduma ya maji ni 147,515 sawa na asilimia 65.0 na kwamba kuna vituo 939 vya kuchotea maji,kati ya hivyo vituo vinavyofanyakazi ni 484.

Anabainisha zaidi kuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru yenye wakazi 256,510,watu wanaopata huduma ya maji ni 164,166 sawa na asilimia 64.0 na kwamba katika Halmashauri hiyo vimejengwa vituo vya kuchotea maji 954 kati ya hivyo vinavyofanyakazi ni 714.

Kwa mujibu wa Meneja RUWASA Mkoa,katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa yenye wakazi146,160,watu wanaopata huduma ya maji ni 73,080 sawa na asilimia 50.0 na kwamba vituo vya kuchotea maji ni 645 kati ya hivyo vinavyofanya kazi ni 312.

Katika Halmashauri ya Madaba yenye wakazi 53,883,idadi ya watu wanaopata huduma ya maji ni 33,407 sawa na asilimia 62.0 na kwamba Halmashauri hiyo ina vituo vya kuchotea maji 419,kati ya hivyo vituo vinavyotoa maji ni 267.

Kulingana na Mhandisi Ganshonga,katika Halmashauri ya Mbinga Mji yenye wakazi 68,338,idadi ya watu wanaopata maji ni 32,500 sawa na asilimia 47.7 na kwamba katika Halmashauri hiyo kuna vituo 305 vya kuchotea maji kati ya  hivyo ni vituo vinavyofanyakazi ni 130.

“Kwa ujumla katika Mkoa wa Ruvuma RUWASA inahudumia wakazi 1,219,642,kati yao idadi ya watu wanaopata maji ni 704,065 sawa na asilimia 57.9,jumla ya vituo vya kuchotea maji ni 4,989,vituo vinavyofanyakazi ni 3065’’,anasisitiza Mhandisi Ganshonga.

Imeandikwa na Albano Midelo

Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa