MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Ahmed Abbas Ahamed akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amezindua zoezi la upandaji miti katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Zoezi hilo limeambatana na ugawaji wa miti kwa wananchi katika Jijiji cha Wino amesema wananchi wa Wilaya hiyo ni wakulima wazuri ikiwa Mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa uzalishaji wa Chakula.
Hivyo Kapenjama amesema kuwa shughuli za kilimo haziwezi kufanikiwa kama mazingira hayatatunzwa kwa ufanisi na kuongeza juhudi ya upandaji wa miti ilikupata mvua za kutosha.
“Hatuwezi kufanikiwa kwenye kilimo miaka inayokuja kama hatutatunza mazingira, kunauwiano wa moja kwa moja kati ya uzalishaji wa chakula kwa wingi na utunzaji wa mazingira jamii ambayo haitunzi mazingira uhai wao wa kuishi ni mdogo sana ”.
Ndile amesema ili mvua iweze kunyesha kwa wingi lazima miti ipandwe kwa wingi ikiwa Serikali imetoa miche bure kupitia Wakala wa Misitu wino ikiwa shamba hilo linalochukua nafasi ya tatu Tanzania kwa ukubwa lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
“Ili tupate mvua nyingi lazima kuwe na miti ya kutosha mfano Nchi ya Kongo,Rungwe,Moshi wana misitu ya kutosha ndiomana wanapata mvua ya kutosha na maeneo ambayo hayana misitu ya kutosha hawanauhakika wa kupata mvua ya kutosha”.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Januari 7,2025
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa