• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

RAIS Samia awakuna wanafunzi kupitia mradi wa SEQUIP

Posted on: February 21st, 2023

MRADI wa SEQUIP umewanifaisha  wanafunzi walioacha masomo kutokana na sababu mbalimbali kuazia miaka 13 hadi 21.

Akizungumza Afisa Elimu ya watu wazima Sekondari  Halmashauri ya Madaba Edward Wellah alipowatembelea wanafunzi hao katika Shule ya Madaba Sekondari,Mahanje na Wino ametoa rai kwa walimu kuwafundisha kama watu wazima bila kujua changamoto zao zilizowafanya wanafunzi hao kuacha masomo yao hapo awali.

“Naomba muwafundishe kama watu wazima bila kuwachapa viboko,kuwafanyisha usafi hata kuwakaripia kwa namna moja au nyingine”

Wellah amewaomba wanafunzi hao kuhudhuria masomo yao kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa saba kamili mchana na kutokata tamaa ikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Watanzania ameona mbali katika swala nzima la kuwapa kipaumbe watoto wa kike kusoma bure kupitia mradi huo.

Amesema mradi huo katika Halmashauri ya Madaba utakuwa katika Shule sita za Sekondari ikiwemo Madaba day,Ifinga,Mahanje,Wino,Ngumbiro na Nguluma.

Kwa upande wake  Mkufunzi John Mapunda  amesema mradi huo utakuwa na hatua mbili ya kwanza watasoma kidato cha kwanza na cha pili na kufanya Mitihani ya Taifa  hatua ya pili watasoma kidato cha tatu na cha nne na kufanya mtihani wa Taifa ya kidato cha nne.

Hata hivyo  Mkufunzi amesema faida za mradi huo kwa wanafunzi ambao watafaulu kuingia hatua ya pili Serikali itawalipia Bima ya Afya na wataendelezwa kusomeshwa.

 “Mjitahidi kusoma hata kama mnaona mda ni mchache mmepata fursa ukiona unachangamoto waoneni walimu na walimu muwasaidie hawa wanafunzi waweze kufikia malengo yao”.

Amesema RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameona kwa jicho la tatu ili kuhakikisha watoto wa kike ambao waliacha masomo yao wanarudi shuleni na kuhakikisha Serikali inawagharamia ada   ili waweze kutimiza malengo yao .

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Madaba

Februari 20,2023.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa