WATUMISHI wa Ifinga Kata ya Matumbi Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma walikuwa wanatumia nusu ya Mshahara wao kwa safari ya kutafuta mawasiliano ya simu.
Wananchi hao walikuwa wanakodi pikipiki kwa shilingi 15,000 hadi eneo lenye mtandao wa simu ilikupata mawasiliano ya mtandao wa simu.
Akitoa historia ya kijiji hicho cha Ifinga kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololeth Mgema amesema kijiji hicho tangu uhuru kilikuwa na changamoto nyingi ambazo sasa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Hassan Suluhu imezipatia ufumbuuzi wa kudumu.
Mgema amezitaja changamomoto hizo ambazo zimekwisha kutatuliwa ikiwemo matengenezo ya Barabara ,Kuweka huduma ya Mawasiliano ya simu ,kuweka huduma ya maji bomba na kuanza mradi wa ujenzi wa kituo cha afya.
“Ifinga ni kijiji pekee mkoani Ruvuma ambacho kipo kilomita 48 kutoka barabara kuu ya Songea –Njombe ambacho kinaunda kata ya Matumbi yenye kijiji kimoja cha Ifinga”.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa