Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile ametembelea na kukagua Zahanai ya Kijiji cha Mbangamawe iliyojengwa kwa Shilingi Milioni 110,000,000/= Kata ya Ngumbiro Halamshauri ya Madaba.
Mganga Mkuu wa Zahanati hiyo Oddo Mapunda amesema katika ujenzi walipokea fedha za ujenzi kutoka Serikali kuu awamu ya kwanza Milioni 50 na awamu ya pili Milioni 50 na nguvu za wananchi Milioni 10.
Mapunda amesema Zahanati hiyo imekamilika kwa asilimia 100 na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Sajidu Idrisa Mohamed amesema bajeti ya mwaka mpya wa Fedha 2023/2024 wataboresha huduma katika Zahanati hiyo kwa kuongeza huduma ya vipimo na Dawa hivyo itatoa huduma ya kiwango cha kituo cha Afya.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halamshauri ya Madaba
Juni 6,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa