• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
MADABA DISTRICT COUNCIL
MADABA DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Department and Section
  • Investment
  • Huduma
    • Huduma ya Kwanza
    • Huduma ya Pili
  • Councillors
  • Miradi
    • Mradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa
    • Matukio
  • Divisheni

MKUTANO wa kuzindua jukwaa la wadau wa usimamizi wa Rasilimali za Maji wazinduliwa Ruvuma

Posted on: November 30th, 2020

KATIBU Tawala msaidizi Jeremiah Sendoro amezindua Mkutano Mkuu wa Jukwaa la wadau wa usimamizi na uendelezaji wa Rasilimali za Maji katika Dakio la sehemu ya juu ya mto Ruvuma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Chritina Mndeme.

Mkutano huo umefanyika  katika ukumbi wa chuo cha Veta Mjini Songea na kuhudhilia wadau mbalimbali  kutoka mikoa mitatu Lindi,Mtwara na Ruvuma.

Akizungumza katika Mkutano huo wa Jukwaa la wadau wa Maji Sendoro amesema ni fursa kwa wadau kujadili na kutoa maoni na mapendekezo ya namna ya kutunza vyanzo vya maji ili visihalibiwe.

Sendoro amesema kwa upande wa  Serikali ya Mkoa wa Ruvuma imejipanga, wananchi wanaoishi sehemu ya mradi huu  itahakikisha unatekelezwa,nakuunda  jumuiya ya watumia maji, sheria za vijiji na Halmashauri ambazo zitalinda watumia maji wote ili asiwepo mtu wa kukosa maji au kupata maji kidogo kulingana na Mahitaji isipokuwa wote wafuate sheria zilizowekwa.

“Tutatoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri,watendaji wa Kata na Makatibu Tarafa na viongozi wote  kuhakikisha wanatekeleza maazimio haya     kwamba wananchi wa Ruvuma  wanapata  Maji na yasichafuliwe wala kupotea bila utaratibu, maji haya tumeyalithi kutoka vizazi vilivyopita nasi tuwalithishe vizazi vijavyo”.alisema Sendoro

Amesema usimamizi na utunzaji wa Rasilimali za Maji kwa mfumo wa mabonde  unasimamiwa na Sheria ya Maji na11 ya mwaka 2009 kusimamia,kupanga,kuendeleza na kutunza Rasilimali za Maji nchi imegawanyika  katika mabonde 9.

Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Ruvuma na Pwani ya kusini  Sudi Mpemba amesema anao wajibu wa kusimamia rasilimali za  Maji katika mabonde na utaratibu waliouanzisha  wa kuzindua  Majukwaa ya Mabonde na  kusimamia Maji umeanza ngazi ya Taifa ni mwongozo wa sera ya mwaka 2002.

Amesema kutakuwa na mwongozo unaelekeza kusimamia Maji ngazi ya Taifa na na ngazi inayoifuata ni Madakio na ndiomana leo tumekutana na wadau kuzindua Jukwaa la  usimamizi wa rasilimali za maji sehemu ya dakio la Mto Ruvuma kwa watumiaji wa sehemu ya juu ndiko kwenye chanzo cha maji sehemu ya matogoro na wanatumia Wilaya ya Mbinga,Songea,Nyasa na Namtumbo

Hata hivyo amesema kupitia jukwaa hili nikuwafanya wadau waweze kuzungumza namna bora ya kusimamia na kuendeleza rasilimali za maji bonde la Maji na kuangalia  changamoto pamoja na kutatua Migogoro .

“Tunatambua watumia maji wapo wa aina mbalimbali kutoka kwenye mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali mfano shamba la kahawa Avivu,watumiaji wanaozalisha umeme,pia kuna wadau wa Halmashauri ya  Mbinga, Nyasa na  tupo hapa kuunda vikundi kwaajili ya usimamizi na tayari umeainisha kwenye mpango wa  usimamizi  na umekamilika na unahitaji kutekelezwa”.amesema mpemba

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumia Maji Bonde la Ndanda Andrew Mwanjela amesema Kwa Mkoa wa Mtwara wamejipanga lakini wanapata changamoto ya uelewa wa  wananchi ni mdogo kwamba chanzo cha maji ni nini? na kutoa visingizio vya Elimu wakati wataalamu wanatoa kila mara,amesisitiza kupitia Jukwaa hili maamuzi yatolewe ili kulinda vyanzo vya maji na kuepuka uhaba wa Maji.

Imeandaliwa na Aneth Ndonde

Afisa Habari Halmashauri ya Madaba

Novemba 30,2020.

Matangazo

  • VIGEZO vya kupata Lesen May 17, 2022
  • Angalia zote

Matangazo Mapya

  • Uboreshaji wa Daftari la kudumu jimbo la Madaba

    January 20, 2025
  • Jitokeze kujiandikisha

    January 20, 2025
  • Chwaya atoa rai kwa walimu wa awali kutekeleza agizo la Serikali

    January 18, 2025
  • MARATIBU wa mradi wa BOOST Madaba amshukuru Rais Samia

    January 18, 2025
  • Angalia zote

Video

WADAU WATOA MAONI JUU YA MAADILI KWA VIJANA
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Ruvuma-webportal
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Nyasa District Council
  • Ega Website
  • Namtumbo District Council
  • Mbinga Town Cuncil
  • Songea District Council
  • Songea Municipal Council

Kurasa Mashuhuru

  • NECTA
  • Tanzania Revenue Authority
  • Tanzania Forest Agency
  • Watumishi portal
  • Livestock Training Agency (LITA) Madaba
  • Parliament

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana Nasi

    MADABA - RUVUMA

    Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA

    Simu: 0252951052

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@madabadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa