Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Wakili Sajidu Idrisa Mohamed, amekabidhi vishikwambi 11 kwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Mhe. Moses Fwiling'afu, leo tarehe 29 Januari 2026 katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Halmashauri. Baada ya makabidhiano hayo, vishikwambi hivyo vilikabidhiwa rasmi kwa Madiwani pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri kwa ajili ya matumizi ya kazi za kiutendaji.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu ya uongozi, kuongeza ufanisi katika upatikanaji na usimamizi wa taarifa za kiutendaji, pamoja na kurahisisha upatikanaji wa nyaraka za vikao na taarifa mbalimbali za maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa