MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amehitimisha maadhimisho ya kilele ya siku ya wanawake Duniani Mkoani Ruvuma.
Maadhimisho hayo yamefanyika kakatika kijiji cha Kalanje katika viwanja vya Baraaza la Idd ,Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma na kauli mbiu ikiwa Wanawake katika uongozi chachu ya kufikia dunia yenye usawa.
“Siku ya leo ni muhimu sana kwa Dunia nzima inaanzimisha siku ya wanawake,ambalo ni tukio muhumu katika jamii yetu kuweza kufahamu umuhimu na nafasi kubwa waliyonayo wanawake katika jamii yetu na katika uongozi wanchi katika kutoa mchango mkubwa wa malezi ya watoto”.
Mndeme amesema wanawake ni nguzo kubwa katika nchi yetu ndio wanaotoa dira na mwelekeo wa maendeleo katika ngazi zote za kifamilia hadi uongozi wa juu ya nchi.
Hata hivyo amesema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na wanawake katika Taifa na kwakuliona hili iliamua kutoa mikopo kwa kuzitaka Halmashauri zote kutenga asilimia 4 ya mapato yake ya ndani ili kuhakikisha wanawake wanawezeshwa.
Amesema Mkoa wa Ruvuma Halmashauri zote kwa kipindi cha Julai 2020 hadi Februari 2021 zimetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 444,167,441.82 kwa vikundi 603 vya wanawake,vikundi 221 vijana vikundi 203 watu wenye ulemavu watu wenye ulemavu vikundi 179.
“Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatekeleza kauli mbiu hii ya Wanawake katika uongozi chachu kufikia dunia yenye usawa hivyo kwa vitendo tunaona wakuu wa Mikoa/Mawaziri,wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi na wakuu wa Idara ambao ni wanawake ni jukumu letu kuwapa wanawake nafasi ya uongozi”.
Afisa maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Ruvuma Zawadi Nyoni akitoa historia fupi ya siku ya wanawake duniani amesema ilianzishwa mwaka 1900 kufuatia maandamano ya wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani kupinga mazingira duni ya kazi.
Nyoni amesema walipinga wakilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira ikiwemo wanawake kulipwa mshahara mdogo kwa kazi sawa ukilinganisha na wanaume.
Amesema wanawake wa Mkoa wa Ruvuma wako mstari wa mbele katika Nyanja za kuleta maendeleo endelevu kwa Jamii ikiwemo kushiriki na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Pia amesema wanawake wamekuwa mstari wa mbele kulaani vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto hususani wa kike,kupinga matumizi ya madawa ya kulevya,na kupambana na janga la UKIMWI na magonjwa ya mlipuko kwa kutumia Elimu kwa jamii kwa njia ya sanaa.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa habari Halmashauri ya Madaba
Machi 9,2021
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa