MBUNGE Viti maalumu anyewakilisha Watumishi Tanzania Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala bora Alice Kaijage ametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kusikiliza kero na changamoto za watumishi.
Akizungumza katika kikao hicho kabla ya kuwasikiliza watumishi hao Kaijage amewapongeza kwa kazi kubwa wanazofanya bila kujali changamoto nyingi wanazo kabiliana nazo katika utendaji kazi.
“Ningeweza kwenda kinondoni lakini nikaona nije Nyanda za juu kusini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba niwaone na niwasikilize ili nikawasemee”.
Hata hivyo Kaijange mara baada ya kuwasikiliza watumishi hao amesema changamoto zote walizozitoa atazifanyia kazi ili kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika mazingira rafiki.
“Bajeti iliyopita kwa miaka mitatu eneo la utumishi halikuachwa na Serikali imeweza kubadilisha miundo na Kada ya watumishi 30,245 na imehuishwa na kusainiwa na kuanzakufanya kazi ilikuwa ni kilio cha miaka mingi”.
Kaijage amesema bajeti ya miaka mitatu watumishi zaidi ya laki nne wamepandishwa madaraja na kugharimu zaidi ya Shilingi Tilioni moja ikiwa upande wa malimbikizo ya mishahara Rais amegusa kwa miaka mitatu na ajira mpya zaidi ya laki moja na ajira elfu 21 Serikali za Mitaa.
“Nasema hayo kwasababu niko kazini Rais Samia ni msikivu amefanya kazi kubwa na anania njema na watumishi”.
Hata hivyo amesema Serikali ya awamu ya sita inagusa kila idara ikiwemo miradi ya Afya na Elimu,na watumishi ikiwa kwa muda wa miaka mitatu ameshusha fedha nyingi katika Halmashauri zote Tanzania hivyo ametoa rai kuendelea kumuunga mkono Rais kwa kufanya kazi kwa bidii.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 15,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa