KAMPUNI ya Tuteinkwa Investment Campany LTD imeanza kuchimba Makaa ya Mawe katika kijiji cha Mtyangimbole Kata ya Mtyangimbole Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Meneja wa Kampuni hiyo Ezekia Makame amesema hadi kufikia sasa wamechimba tani 5,000 ambapo mwisho wa mwezi Nomba 2023 wanatarajia kusafirisha mara baada ya ukamilishaji wa Barabara inayotoka katika mgodi huo na kufika katika Barabara kuu.
Hata hivyo Makame amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Sajidu Idrisa Mohamaed kwa kutoa ushirikiano kuanzia kampuni hiyo inaanza kufanya utafiti hadi kufikia kuanza uchimbaji wa Makaa ya Mawe.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Ndile ametembelea eneo la mgodi, ameipongea Kampuni hiyo kwa kuanza zoezi la uchimbaji na upanuzi wa Barabara yenye kilomita 35 ambayo pia itawasaidia wananchi katika shughuli zao za uchumi.
Ndile mara baada ya kukagua Mgodi huo wa uchimbaji wa Mkaa ya Mawe amehaidi kutoa ushirikiano katika utatuzi wa changamoto zilizobaki ikiwemo Barabara na kuhakikisha makaa hayo ya Mawe yanaanza kusafirishwa kwa wakati uliopangwa.
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
Novemba 02,2023.
MADABA - RUVUMA
Anwani ya Posta: 38 BARABARA YA KIFAGURO MAGINGO, P.O.BOX 10, 57186 MADABA, SONGEA
Simu: 0252951052
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@madabadc.go.tz
Hatimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.Haki zote zimeifadhiwa